Chanzo kutoweka mwandishi hadharani

07Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Chanzo kutoweka mwandishi hadharani

Baada ya kupotea kwa takribani siku 17 mwandishi wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi, Azzory Gwanda, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Francis Nanai amesema japo hawana uhakika na sababu za watu wasiojulikana kumteka mwandishi wao, inawezekana kuandika habari za mauaji ya Kibiti ikiwa chanzo.

Azzory Gwanda.

Akizungumza na wanahabari leo Disemba 7 katika ofisi ya gazeti hilo, Nanai amesema hawajui sababu maalumu ya kupotea kwa mfanyakazi wao ila wanachoamini wakimpata akiwa hai watapata sababu za kutosha.

"Siwezi kusema sababu za kupotea kwa ndugu yetu Azorry, lakini inawezekana kutokana na ripoti alizokuwa akizifanya kutokana na mauaji yaliyokuwa yakifanyika Kibiti ikawa sababu ya kukamatwa kwake, lakini pengine tukimpata anaweza kutupa mwanga wa sababu za kukamatwa kwake". Nanai

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi, Francis Nanai akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tukio la kutoweka kwa wandishi wa kampuni  hiyo Azzory Gwanda. 

Aidha Nanai ameongeza kwa kusema kwamba Mwandishi wao Azzory hakuwahi kuripoti kuhusu kutishiwa amani au kufuatiliwa kwa namna yoyote ndiyo maana hawajui sababu ya kuchukuliwa na watu hao ni nini.

 

Habari Kubwa