Cheyo amshauri Magufuli kongamano vyama vya siasa

12Jul 2020
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Cheyo amshauri Magufuli kongamano vyama vya siasa

MWENYEKITI wa Chama cha UDP, John Cheyo, amemshauri Rais Magufuli, kufikiria uwepo wa kongamano la vyama vya siasa nchini ambalo litajumuisha vyama vyote vya upinzani kwa lengo la kujadili masuala muhimu ya Kitaifa.

Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo.

Mbali na hilo, pia mwenyekiti huyo amemuomba Rais Magufuli kuwezesha kuwepo kwa uwakilishi wa wabunge wakulima watakaopaza sauti kwa ajili ya wakulima wa mazao mbalimbali yanayoulimwa nchini ili yaweze kuuzwa kwa bei nzuri na mkulima afaidike.

Aidha, Cheyo amerudia kauli yake kuwa UDP inaendelea kuunga mkono Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu hususan katika nafasi ya Urais.

Habari Kubwa