Chui akutwa na maambukizi ya corona

06Apr 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Chui akutwa na maambukizi ya corona

Chui wa kike mwenye umri wa miaka minne anayefungwa katika bustani ya wanyama Marekai amemekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

chui nadia.

Chui huyo ameweka rekodi ya kuwa mnyama wa kwanza kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo duniani. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya vya Marekani, chui huyo alikuwa akiishi katika Bustani ya Bronx iliyopo katika mji wa New York, Marekani.

“Matokeo hayo yalithibitishwa na maabara ya huduma ya afya ya mifugo mjini Lowa,” limeandika Shirika la Utangazaji la BBC.

Kwa mujibu wa BBC, chui huyo mwenye asili ya Malaysia ametambulika kwa jina la Nadia, pamoja na wengine wawili pamoja na simba watano wa Afrika walianza kuwa na kikohozi kikavu mwishoni mwa wiki.

“Baada ya vipimo chui huyo aligundulika kuwa na maambukizi na tayari ameshaaza matibabu,” imesema taarifa ya viongozi wa bustani hiyo.

Uongozi huo umesema kuwa inaaminika chui huyo aliambukizwa na mmoja wa wafanyakazi katika bustani hiyo. Bustani hiyo imesema haijui virusi hivyo vitawaathiri vipi wanyama wengine kama simba lakini kwa sasa wamewaweka chini ya uangalizi.

Chanzo: BBC

Habari Kubwa