Chuo cha usimamizi wa fedha kujengwa Simiyu

18Jun 2019
Happy Severine
BARIADI
Nipashe
Chuo cha usimamizi wa fedha kujengwa Simiyu

Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof  Thadeo Sata amewahakikisha wakazi wa Kanda ya Ziwa na Magharibi, ujenzi wa awali wa Tawi la chuo hicho katika kijiji cha Sipiwi mkoani Simiyu, kukamilika  mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kudahili wanafunzi wapatao 10,000.

makamu mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha Thadeo Sata (aliyevaa suti) akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ramani ya ujenzi wa chuo cha usimamizi wa fedha kinachohenga katika kijiji cha Sapiwi Mkoani Simiyu.

Haya yamesemwa leo na  Prof Sata wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa tawi la Chuo cha usimamizi wa fedha katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi.

Prof Sata amesema, Tawi la Sapiwi Mkoani Simiyu ni fursa kubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa ambao walikuwa wakifuata huduma  zao katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Dar es salaam.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  Anthony Mtaka amesema uamuzi wa IFM wa kujenga tawi  Mkoani mwake, ni uamuzi sahihi  ,huku akitoa wito kwa wananchi kujenga hosteli kwa wingi zitakazoweza kuwahudumia wanachuo wote.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha sapiwi wameshukuru  uwepo wa ujenzi huo kwani umeanza kuwapatia ajira .

Msimamizi wa ujenzi huo kutoka Chuo cha mafunzo ya ufundi veta  Kagera Baluye Mitinje   ameahidi kujenga usiku na mchana  ili kuhakikisha wanamaliza kwa wakati

Ujenzi wa awali wa Chuo cha usimamizi wa fedha tawi la sapiwi utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia Tisa na sabini na Moja.

Habari Kubwa