COSTECH yatoa Milioni 296 kuwezesha utafiti wa kilimo

16Apr 2019
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
COSTECH yatoa Milioni 296 kuwezesha utafiti wa kilimo

TUME ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa kiasi cha Sh.Milioni 296.906 kwa Taasisi  ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI),Makutupora Dodoma, ili kununua vifaa vya kisasa vya maabara kwa ajili ya utafiti  wa kilimo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kituo hicho, Dk. Cornel Masawe, fedha hizo zimetumika katika kukarabati wa maabara,ikiwa ni sehemu ya mpango maalum ulioanzishwa na kituo.

Amesema baada ya kukamilisha, maabara hiyo itafanya jukumu la kuwawezesha wazalishaji wa mvinyo kutengeneza chupa za ubora wa kiwango cha juu kuendana na kasi ya viwanda.

"Tuna imani kuwa wakulima wakikitumia vizuri kituo hiki , kitasaidia kuzalisha zabibu na kuzalisha zabibu yenye sukari ya kiwango cha juu ambacho   kimependekezwa katika ubora ili kuwezesha viwanda vya ndani kutengeneza mvinyo bora," amesema

Kwa upande wake, Msimamizi wa Makundi ya zabibu ya Mizabibu ya Kati, Richard Malle, amewahimiza wakulima kutumia wataalamu kutoka kituo hicho  ili waweze kulima zabibu bora.