"Damu ya Mtanzania haipotei"- IGP Sirro

15Jul 2019
Na Mwandishi Wetu
GEITA
Nipashe
"Damu ya Mtanzania haipotei"- IGP Sirro

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Sirro, amemuhakikishia Rais John Magufuli amani, usalama na utulivu kuendelea kutawala nchini.

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Sirro.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa uzinduzi wa nyumba 20 za askari uliofanyika Wilaya ya Magogo katika Mkoa wa Geita. Sirro amemuelezea Mhe Rais Magufuli tukio la mauaji ya watanzania yaliofanyika nchini Msumbuji hivi karibuni na kusema kuwa watu watano wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo wanashikiliwa kwa uchunguzi huku mmoja wao akiwa amefariki.

"Lile tukio lililonipeleka Msumbiji, niliahidi kwa Watanzania kwamba damu ya Mtanzania haipotei, nikuhakikishie Mhe. Rais hadi sasa watano wameshakamatwa na mmoja ameshatangulia mbele za haki (kufa), na hao wanaoshikiliwa watataja yote waliyokua wakiyafanya hapa kwetu,"amesema Sirro

Katika hatua nyingin, Sirro amemueleza Rais Magufuli kuwa kumekuwa na upungufu mkubwa wa matukio ya uhalifu kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na mwaka huu, amemshukuru Rais kwa kukubali mualiko wake wa kutuzindulia nyumba 20 ni muhimu na zitaongeza morali kwa askari.

Aidha amemuomba Magufuli kuruhusu jina lake litumike katika kambi hiyo yenye karibu heka 19, kwani anaamini masuala yote ya kijeshi yatafanyika katika kambi hiyo na kama itafaa kambi hiyo ijulikane kwa jina "John Pombe Magufuli Police Barracks".

" Mhe. Rais niombe kitu kidogo tu ingawa si kawaida yangu..Ukubwa wa kambi yetu ni karibu heka 19, naamini masuala yote ya kijeshi yatafanyika hapa, kama itafaa basi jina lako lionekane kama John Pombe Magufuli Police Barracks, tutafarijika sana", amesema Sirro

Habari Kubwa