Dawa bandia, duni bado tishio Afrika 

14Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Dawa bandia, duni bado tishio Afrika 

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, amesema uzalishaji na matumizi ya dawa bandia na sizizo na viwango ni tatizo kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya nchi za Afrika.

duka la dawa.

 Amesema ni muhimu nchi za Afrika kuweka mikakati inayolenga kukomesha uzalishaji na matumizi ya dawa hizo kwa kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha dawa zinazotumiwa na waafrika zina ubora unaotakiwa.

Dk. Ndugulile alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Dawa Afrika (African Medicines Quality Forum—AMQF).  

Mkutano huo uliandahiliwa na Shirika la Maendeleo Afrika (NEPAD), The United States Pharmacopeia Convention (USP), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

Kwa mujibu wa Waziri Ndugulile, dawa bandia na sizizo na viwango ni tatizo kubwa barani Afrika, linalohitaji mikakati madhubuti na kwamba mikakati haiwezi kufanikiwa bila ushiriakiano wa wadau wote.

 

 

Habari Kubwa