Dawasa kumaliza kero ya maji Kimara Golani

15Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Dawasa kumaliza kero ya maji Kimara Golani
  • * Ni ndoto ya muda mrefu imepata majibu
  • * Dawasa yajigamba kufikisha huduma kwa wananchi kwa asilimia 95 ifikapo Desemba 2020

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma Ubungo imeanza utekelezaji wa kazi ya ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji katika eneo la Kimara Golani lililokosa huduma ya maji safi kwa kipindi kirefu.

Mafundi wa dawasa wakiendelea na zoezi la ulazaji bomba.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa DAWASA Mkoa wa Ubungo Mhandisi Pascal Fumbuka ambapo ameeleza kuwa kazi inayoendelea hivi sasa ni ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji ya ukubwa wa inchi 2, 3, 4, 6, 8 na 9 kwa urefu wa kilomita 20.

“Eneo la Kimara Golani limekuwa na tatizo la huduma ya maji kwa kipindi kirefu hivyo kama DAWASA Ubungo tukaliweka katika maeneo ya utekelezaji kwa mwaka huu wa fedha ambapo mradi ukikamilika utaenda kuhudumia kaya takribani 4,000 katika eneo hilo,” amesema Fumbuka.

DAWASA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji maji katika maeneo tofauti ya Mkoa Dar es salaam pamoja na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani ikiwa ni moja ya juhudi zakufikia asilimia 95 za upatikanaji wa maji ifikapo Desemba, 2020.

Habari Kubwa