Dawasa yaanza kutoa leseni,kusajili magari ya kusambaza maji

15May 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Dawasa yaanza kutoa leseni,kusajili magari ya kusambaza maji

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) leo imeanza zoezi la kusajili na kutoa leseni za uendeshaji kwa wamiliki na waendeshaji wa magari ya kusambaza majisafi (Water Bowsers).

Afisa kutoka dawasa akitoa maelekezo kwa dereva wa gari la kusambaza maji baada ya kubandika stika ya dawasa katika gari lake kama ishara ya kutambulika.

Kwa mijibu wa taarifa kutoka Dawasa, imesema lengo la usajili huo ni kuhakikisha wateja wanaopata maji kupitia magari hayo wanapata huduma bora kutoka vyanzo rasmi vya maji vinavyotambuliwa na DAWASA.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa matenki ya magari yatakayokidhi vigezo vya kupata usajili yatasafishwa na yatawekewa  dawa maalumu ya kuua wadudu kwenye matanki ya gari  na kubandikwa stika za DAWASA. 

"Baada ya muda wa usajili kuisha, gari yoyote ya Majisafi itakayokutwa katika eneo la huduma la DAWASA ikitoa huduma bila leseni ya uendeshaji, itachukuliwa hatua kali za kisheria.Wananchi wanashauriwa kutumia Magari ya kusambaza Majisafi yaliyosajiliwa na DAWASA kuepukana na usumbufu".

Usajili na utoaji leseni za uendeshaji litafanyika katika eneo la Chuo Kikuu Ardhi kwenye matanki ya DAWASA Maarufu kama (Terminal). Gharama ya usajili ni Tsh 100,000/= (itakayolipwa baada ya kukamilisha vigezo vyote

Taarifa zinazotakiwa kwa ajili ya usajili huo ni:

1. Picha moja ya rangi ya mmiliki wa gari na nakala ya kitambulisho chake (KURA, UTAIFA AU HATI YA KUSAFIRIA)

2. Nakala ya kadi ya gari, nakala ya bima ya gari na nakala ya leseni ya dereva  (vithibitishwe na Mwanasheria)