DAWASA yafanya mabadiliko mzunguko usomaji mita za maji

02May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
DAWASA yafanya mabadiliko mzunguko usomaji mita za maji
  • Bili sasa kutumwa kwa wateja kati ya tarehe 20 hadi 30 kila mwezi...

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema kuanzia mwezi Mei mwaka huu itafanya mabadiliko katika mzunguko wa usomaji mita na utumaji wa Ankara za maji (bili) kwa wateja wake.

mita ya maji.

Taarifa iliyotolewa leo Mei 02,2021 kwa umma na Kitengo cha Mawasiliano na Jamii DAWASA, imesema kuwa mabadiliko hayo yanawahusu wateja wa Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Kihaba, Bagamoyo, Chalinze, Kisarawe na Mkuranga mkoani Pwani.

"DAWASA imefanya mabadiliko katika mzunguko wa usomaji mita na utumaji wa Ankara za maji (bili) kwa wateja wake kutoka tarehe 1 hadi 15 ya kila mwezi kwenda tarehe 20 hadi 30, mabadiliko haya yataanza mwezi Mei mwaka huu, hivyo basi ankara za maji kwa mwezi Mei, zitaanza kutumwa kwa wateja kuanzia tarehe 20 hadi 30.," imeeleza taarifa hiyo

DAWASA imesisitiza kuwa mteja anatakiwa kuilipa Ankara (bili) ndani ya siku 30 kuanzia siku ya kwanza uliyopokea ankara hiyo.Pia DAWASA inawakumbusha wateja wake kulipia malimbikizo ya madeni yao ya kipindi cha nyuma ili kuiwezesha mamlaka hiyo kuboresha huduma zake.

 

Habari Kubwa