DAWASA yatoa elimu usomaji mita na ulipaji ankara za maji

23Feb 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
DAWASA yatoa elimu usomaji mita na ulipaji ankara za maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la kutoa elimu ya usomaji wa mita za wateja na namna ya kulipa ankara za maji kupitia mifumo mbalimbali ya  mawasiliano ya kielektroniki.

Zoezi hilo linalenga kuhamasisha wateja wanaohudumiwa na DAWASA kujua matumizi sahihi ya bili zao na kuona umuhimu wa kulipa ankara kwa muda sahihi ili kuepuka usumbufu.

Utekelezaji wa zoezi hili unafanyika leo katika  maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam yanayohudumiwa na DAWASA kwa watumishi wa mamlaka hiyo kukutana na wateja kwenye makazi yao na kuwapa elimu hiyo.

Wateja waliofikiwa wametoa ushirikiano kwa mamlaka kwa kulipa ankara zao papo hapo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano zaidi wa kufanikisha ulipaji wa ankara za maji kwa wakati.

Mamlaka ilitoa elimu kwa wateja wake na kuwaelewesha kuwa ulipaji wa ankara za maji ni muhimu kwa kuwa huiwezesha mamlaka kuboresha huduma na kutekeleza miradi mbalimbali ya maji yenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wengine.

Habari Kubwa