DC ameionya TARURA kukaa ofisini madaraja yakisombwa na maji

20Mar 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
DC ameionya TARURA kukaa ofisini madaraja yakisombwa na maji

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameagiza wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) mjini humo, kuacha tabia ya kukaa maofisi bali wafanye ukaguzi wa madaraja na kuyafanyie matengenezo, yale ambayo yanaonekana kuharibika na siyo kusubili hadi yasombwe na maji na kukata mawasiliano.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kulia aliyevaa kofia Akitoa maelekezo kwenye daraja la kijiji cha Uzogole Shinyanga.

Mboneko alibainisha hayo jana wakati akikagua daraja lililosombwa na maji katika kijiji cha Uzogole Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, pamoja na barabara ya Mwawaza ambayo imekatwa na maji na kusababisha usumbufu kwa wananchi kupita ndani ya maji, na kuhatarisha maisha yao.

Alisema kwenye kipindi hiki cha mvua ni vyema watendaji wa wakala hao wa barabara vijijini na mijini, waache tabia ya kukaa maofisi bali wafanye ukaguzi wa madaraja yote ambayo yapo katika hatari ya kusombwa na maji wayafanyie matengezo mapema, na siyo kusubili hadi ya bomoke ndipo waanze kutengeneza.

“Naagiza kuanzia sasa watendaji wote wa wakala wa barabara vijijini na mijini TARURA muache tabia ya kukaa maofisini, bali nendeni field mkague madaraja yote pamoja na barabara ambazo zimeshaharibika na kuzifanyie matengenezo, na siyo kusubili hadi zisombwe na maji na kukata mawasiliano kwa wannachi,”alisema Mboneko.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko aliyevaa kofia, akiangalia ufukiaji wa mabomba kwenye mradi wa maji Ziwa Victoria yanayopelekwa Kata ya Masengwa wilaya ya Shinyanga, wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Wakala wa Maji Vijijini na Mijini Wilaya ya Shinyanga (RUWASA), Emmael Mkopi.
Mhandisi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (Shuwasa) ambaye ni Meneja ufundi, Yusuph Katopola, akiingiza namba ili kununua maji kwenye mita ya maji kama mfumo wa Luku, kwenye mradi wa Lubaga ambao wameshamaliza kuutekeleza, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, akifungua maji ya mradi wa Ziwa Victoria katika eneo la Lubaga Shinyanga uliomaliza kutekelezwa na Shuwasa kwa gharama ya Shilingi Milioni 15, kushoto ni Mhandisi wa Shuwasa Yusuph Katopola. 

“Madaraja yote ambayo yamesombwa na maji pamoja na barabara zilizokatika, naagiza mzitembelee na kuzifanyia matengenezo haraka, ili wananchi wapite kwa usalama na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kuto hatarisha maisha yao tena,”aliongeza.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Uzogole, Peter Digo, alisema daraja la kwenye kijiji hicho lina wiki moja limekatika na kukata mawasiliano, huku wananchi wakipita hivyo hivyo ndani ya maji ambayo yanapita kwa kasi na kuhatarisha maisha yao, sababu hakuna njia nyingine mbandala ya kupita.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TARURA Manispaa ya Shinyanga, Maige Kulwa, alisema kwenye barabara ya Mwawaza ambayo imekatwa na maji tayari wameshatenga Shilingi Milioni 12 kwa ajili ya kuifanyia matengezo, huku daraja wa Uzogole wataomba fedha ili walifanyie  nalo matengenezo.

Wananchi wakipita ndani ya maji kwenye barabara ya Mwawaza Shinyanga ambayo imekatwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kushoto akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Vijijni na Mijini Tarura, Manispaa ya Shinyanga Maige Kulwa.

Muonekano wa Daraja la Uzogole Shinyanga likiwa limesombwa na maji na kukata mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kulia akikagua daraja la Kijiji cha Uzogole lililopo Kaya ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga ambalo limesombwa na maji na kukata mawasiliano.

Habari Kubwa