DC aridhishwa ujenzi Majengo chuo cha Ualimu

15Sep 2021
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
DC aridhishwa ujenzi Majengo chuo cha Ualimu

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekagua ujenzi na ukarabati wa majengo, katika chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), na kuagiza Mkandarasi akamilishe mapungufu yaliyopo zikiwamo nyufa.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ujenzi wa Madarasa katika chuo cha Ualimu SHYCOM.

 

Mboneko amefanya ziara hiyo jana, akiwa ameambata na viongozi wa Serikali, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sanyansi na Teknolojia, ilitoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 9.8  kwa ajili ya kukarabati na kujenga majengo katika chuo hicho cha Ualimu Shycom, ili kuboresha mazingira mazuri ya kusomea wanafunzi.

"Leo nimefanya ziara ya kukagua maboresho na ujenzi wa majengo katika chuo hiki cha Ualimu Shycom, ili kuona maendeleo yake, na kuhakikisha kama wanafunzi wameanza kuyatumia," alisema Mboneko.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua miundombinu ya choo chuoni hapo.

"Serikali tumekarabati na kujenga Mabweni, Madarasa, vyoo, nyumba za walimu, bwalo, maktaba ya vitabu, jengo la midahalo,pamoja kujenga tenki la Maji lita 300,000 , na kumaliza changamoto ya maji chuoni hapo," aliongeza.

Pia, amewataka wanafunzi katika chuo hicho, kuyatunza majengo hayo,kuimarisha mazingira ya usafiri, pamoja na kusoma kwa bidii, ili waje kuwa Walimu Wazuri na Kufaulisha wanafunzi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, akikagua miundombinu ya choo chuoni hapo.

Naye Mkuu wa chuo hicho cha Ualimu John Nandi, amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kupambana kukikarabati chuo hicho, na kubainisha kuwa kwa sasa kinavutia, na idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 500 hadi 700.

Alisema ujenzi na ukarabati wa Majengo chuoni hapo ulianza mwaka 2016 na umekamilika May mwaka huu, ambapo tayari majengo hayo yameanza kutumiwa na wanafunzi.

Nao baadhi ya wanafunzi chuoni hapo akiwamo Leokadia Cosmas, wameipongeza Serikali kwa kuwaboreshea mazingira mazuri chuoni hapo, huku wakiahidi kuyatunza majengo hayo pamoja na kusoma kwa bidii.

Habari Kubwa