DC Babu aagiza fedha kutengwa mafunzo ya mgambo

07Dec 2021
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
DC Babu aagiza fedha kutengwa mafunzo ya mgambo

MKUU wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha Nurdin Babu ametoa agizo kwa Halmashauri ya Longido kutenga fedha kipindi Cha kupanga Bajeti kwa ajili ya kuendeshea Mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo).

"Askari  hawa ni wa halmashauri, hivyo mtakavyoanza kutenga bajeti mwakani mwezi wa pili ,tengeni fungu la jeshi la akiba" amesema Babu.

Babu, amesema hayo alipokuwa akihitimisha mafunzo ya jeshi  la akiba  yaliyochukua takribani miezi minne katika Kata ya Engarenaibor, nakueleza kuwa jeshi linahitaji watu wenye nidhamu na weledi,nakuwahasa kutokubali kushawishiwa na watu wenye nia hovyu kwa sababu wamewaona wamepata mafunzo mazuri. 

"Mmejifunza kushika silaha ,pamoja na jinsi ya kufunga na kufungua silaha  na mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Uhamiaji,TAKUKURU,Usalama wa raina hata usalama wa Taifa hivyo mmeongeza ujuzi,mkawe wazalendo kwa nchi yetu" ameeleza Babu.

Amefafanua kuwa,wilaya hiyo imejipanga kuanzisha mfuko wa maendeleo kwa jeshi la akiba ambao wadau na watu wengine watakaoguswa watachangia fedha kupitia Mfuko huo kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.

" Nimeona hapa mmesema mlianza mafunzo mkiwa 76 na leo mnahitimu mkiwa 51, wengine walishindwa kuendelea  kutokana na kukosa fedha za sare ya jeshi la akiba, naanza kwa kuchangia Shilingi. 500,000 kwa ajili ya sare ya jeshi la akiba kwa mafunzo ya jayo." alisema Babu.

Habari Kubwa