DC Babu atoa wito wananchi kujikinga na corona

29Jul 2021
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
DC Babu atoa wito wananchi kujikinga na corona

MKUU wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, Nurudin Babu ametoa wito kwa wananchi wilayani humo kuchukua tahadhari zote dhidi ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO -19 kwa kufuata miongozo yote ya kiafya.

MKUU wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha Nurudin Babu.

Alisema hayo alipokua katika ziara ya kikazi kwenye Kata ya Olmolog na Kamwanga Tarafa ya Enduiment jana, alisema kata hizo ni  kata zilizopo pembezoni na mpaka wa nchi jirani ya Kenya, hivyo mwingiliano ni mkubwa wa watu.

" Fuateni taratibu zote za kiafya ikiwemo kuvaa barakoa , kutumia vitakasa mkono na kuepuka misongamano" alisema Babu.

Babu aliwataka wananchi wilayani humo kuepukana na maneno ya upotashaji dhidi ya chanjo ya corona inayotolewa na kusema kuwa hakuna serikali inaweza kutoa chanjo kwa lengo la kuua wananchi wake.

" Epukeni maneno ya upotashaji chanjo ni salama kabsa,na hata itakapofika Longido nitakuwa wakwanza kuichoma mimi mkuu wenu wa wilaya, lakini pia mmeona kupitia vyombo vya habari Rais Samia na kamati yake ya ulinzi ya Taifa wamepata chanjo tayari" alisema Babu