DC Ikungi aridhishwa ujenzi madarasa

06Dec 2021
Faustine Feliciane
DAR ES SALAAM
Nipashe
DC Ikungi aridhishwa ujenzi madarasa

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jerry Muro amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari hususani kata ya Mkiwa iliyopo Halmshauri ya wilaya hiyo.

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jerry Muro.

Akizungumza na Nipashe Digital kwa njia ya simu, Muro amesema amefanya ziara kwenye miradi ya ujenzi wa shule na kuridhika na kasi ya ujenzi huo na anategemea madarasa hayo kukamilika Desemba 15.

"Nimefanya ziara kwenye kata ya Mkiwa nikiwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri na pia diwani wa kata ya Mkiwa, nimeridhishwa na kasi ya ujenzi na naamini ifikapo Desemba 15 tutakabidhiana madarasa haya," amesema Muro.

Amesema kuwa lengo la ziara yake kwenye miradi ya ujenzi wa madarasa wilayani mwake ni kujaribu kuondoa changamoto yoyote itakayojitokeza na kutishia au kukwamisha ujenzi.

"Hatutaki kuona ujenzi unasimama au unakwamishwa na kitu chochote na ndio maana tunazunguka kila wakati kuona nini kinaendelea, tunataka miradi yote ikamilike kwa wakati," amesema Muro.

Amesema lengo la Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuweka mazingira bora ya kupata elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa na miundo mbinu mingine.

Amesema wilaya yake itekeleza mrasi wa ujenziwa vyumba vya madarasa 67 vya shule za sekondari na madarasa 65 ya shule shikizi na msingi.

Habari Kubwa