DC Joketi aagiza watendaji TANESCO kuswekwa ndani

17Jan 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
DC Joketi aagiza watendaji TANESCO kuswekwa ndani

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo, ameagiza kuswekwa mahabusu baadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilayani humo, baada ya kukithiri kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utolewaji wa huduma duni.

Alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za TANESCO Wilaya ya Kisarawe na kukuta idadi kubwa ya wananchi waliofika kutoa malalamiko kutokana na kukosa huduma ya nishati ya umeme kwa wakati.

Akizungumza katika ofisi hizo, Jokate alisema hawezi kukubali kuona wananchi wakiendelea kulalamika kuhusu kukosa huduma ya umeme, huku baadhi ya watendaji wakipuuza na kuwadharau wananchi.

Alisema sababu kubwa ya kuwapo kwa malalamiko mengi ya wananchi inatokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watendaji na watumishi wa TANESCO.

"Kuna watendaji wanapenda rushwa na matokeo yake wanakwamisha huduma kupatikana kwa wakati unaotakiwa,” alisema Joketi huku akitoa amri kwa polisi kuwakamata baadhi ya watendaji na watumishi wa Shirika hilo na kuwaweka rumande wajitafakari wakiwa huko.

"Wanaohusika wote na kutoa huduma kwa wateja wapelekwe kituo cha polisi watafakari utendaji wao wa kazi na maisha yao.”

"Haiwezekani wananchi wawe wanalalamika kila siku kuhusu huduma za TANESCO hapa Kisarawe, tumekuwa tukizungumza mara nyingi kwenye vikao vyetu, lakini wenzetu hamtaki kusikia wala hamfanyii kazi malalamiko ya wananchi,” alisema Joketi na kuongeza:

"Sasa niwaambie mimi niko na wananchi, malalamiko ni mengi, tunakubaliana na humfanyi kazi, nachukua haya malalamiko na kuyafikisha kwa Mtendaji Mkuu wa TANESCO maana ninyi hapa mmeshindwa kuyafanyia kazi, huduma kwa wateja mbovu,” alisema Joketi.

Akitoa mfano, Joketi alisema kuna mmoja wa mwananchi ambaye anaishi karibu na ofisi za TANESCO na alipopata tatizo la hitilafu ya umeme kwenye nyumba yake ilichukua zaidi ya mwezi mmoja pasipo kupata msaada wowote...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa