DC Kigoma awataka wananchi kuacha kuharibu mazingira kwa makusudi

21Nov 2021
Adela Madyane
Kigoma
Nipashe Jumapili
DC Kigoma awataka wananchi kuacha kuharibu mazingira kwa makusudi

​​​​​​​MKUU wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe, amewataka wananchi kuacha tabia ya uharibifu wa mazingira na kusingizia mabadiliko ya tabia nchi.

Ameyasema haya leo Novemba 21, 2021 katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya mvuvi duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Acqua lodge mkoani Kigoma.

Amesema nchi ipo kama ilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu ila shughuli za kibinadamu za ukataji miti na uharibifu mwingine wa mazingira ndio hasa chanzo cha kuiharibu nchi.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wanandamu kuacha kuharibu mazingira kwa makusudi kwa kuwa jambo hilo litazidi kuharibu mazingira na kuteketeza rasilimali zilizopo.

Habari Kubwa