Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk Severine Lalika alipokuwa akizungumza leo na Nipashe ofisi kwake, amesema kuwa mimba zimekuwa vikwazo kwa watoto wa kike kukatisha masomo yao.
Amesema amepokea kesi nyingi hasa kipindi cha likizo ya corona hasa katika kata za mjini ikiwemo Kirumba, Kitangiri na Sangabuye hivyo kamati hiyo itasaidia kuondokana na tatizo hilo.
"Kata ya Kawekamo imekuwa na kamati hiyo imesaidia sana kwani inaundwa na watu mbalimbali wakiwemo walimu , maofisa ustawi wa jamii, viongozi wa kijamii na wamekuwa wakifatilia shule kwa shule kubaini kama kuna mimba ,kuwachukulia hatua waliosababisha na kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wanafunzi,"amesema Dk Lalika.
Ameongeza kuwa tatizo kubwa ni wazazi kutokutoa ushirikiano pindi kesi zinapoenda mahakamani hivyo aliwataka wazazi kutoa ushirikiano ili haki itendeke na wahusika wachukuliwe hatua.
Amesema ukinzani wa kisheria ni tatizo hasa binti anapogeuka mahakamani kumlinda aliyempatia ujauzito ambapo ukisema usubilie mtoto azaliwe ili kupima vinasaba kwa upande wa sheria hairuhusu upimaji wa vinasaba(DNA) kwa mtoto mchanga mpaka afikishe miezi 7 .
Amesema kesi hiyo itachukua muda mrefu na wazazi wa binti wanakata tamaa na kuona mtoto atashindwa kuhudumiwa na kuridhia makubaliano na mtuhumiwa hivyo utaratibu wa kisheria uboreshwe kwa kuwa na utaratibu wenye kusababisha waliosababisha madhara wachukuliwe hatua ikiwemo kufungwa.