DC Maswa azindua bodi ya kusimamia viwanda

13Aug 2020
Happy Severine
Maswa
Nipashe
DC Maswa azindua bodi ya kusimamia viwanda

MKUU wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, Aswege Kaminyongi, amezindua bodi ya kampuni ya Ng'hami(Ng'hami Industries Compay Ltd) ambayo itaendesha viwanda vinavyomilikiwa na halmshauri hiyo.

Akizindua bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya Maswa mkuu huyo amesema uzinduzi wa bodi hiyo unaashiria utekelezaji wa dhamira njema ya kuwa na viwanda vya kimkakati ndani na nje ya Mkoa wa Simiyu.

Kaminyongi amesema matokeo ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa sekta ya viwanda Wilayani Maswa yameanza kuonekana dhahiri kwa vitendo na kukuza uchumi wa wananchi wao kwa ujumla.

Bodi hiyo itasimamia viwanda vitano ambavyo ni kiwanda cha kusindika unga lishe wa viazi, kiwanda cha chaki, kiwanda cha vifungashio, kiwanda cha unga wa gypsum na cha kutenga madaraja ya mchele.

Habari Kubwa