DC Misungwi apewa mtego ujenzi Hospitali ya Wilaya

29Jun 2020
Neema Emmanuel
Mwanza
Nipashe
DC Misungwi apewa mtego ujenzi Hospitali ya Wilaya

​​​​​​​MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Misungwi kufanya vitu tofauti katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo kwa kuongeza nguvu zaidi.

Mongella ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi huo, huku akisifia kazi inayoendelea ni nzuri lakini waongeze nguvu kwani fedha za Force Account zinatumika ndani ya siku 90 na ujenzi uwe umekamilika.

"Huko nyuma yalifanyika mauzauza na wengine tulishiriki Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi tufikiri tofauti kuongeza kasi na kufanyia vitu vya tofauti ili kuwatofautisha na wengine ambavyo vitakuwa kumbukumbu ata mtu akiona anasema fulani alifanya hiki chamsingi tuwe waadilifu na tupige kazi na kukaza buti na tufanye vitu vya tofauti" amesema Mongella.

 

 

 

 

 

Pia Mongella amewaomba wananchi kuendelea kuvilinda vifaa vinavyotumika katika ujenzi sambamba na kufanyia kazi kwa sababu fedha hizo za ujenzi zimetolewa na Rais Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dr Zabron Masatu, amesema fedha iliyopokelewa katika awamu ya kwanza Million 500 (500,000,000) imeelekezwa kujenga majengo matatu ambayo ni jengo la OPD, jengo la maabara na kichomea taka.

"Hospital hii ikikamilika  itahudumia wananchi wa eneo hili wapatao 462,855 ,pia uongozi wa Wilaya kwa niaba ya wananchi tunatoa shukrani nyingi kwa serikali hii inayoongozwa na Magufuli kwa kuwezesha ujenzi wa  kihistoria wa hospital ya wilaya,tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana nasi katika kuleta maendeleo ya jamii kuelekea uchumi wa kati" amesema Masatu.

Habari Kubwa