DC Mwaisumbe aagiza msako wafugaji waliopiga watendaji Longido

28May 2019
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
DC Mwaisumbe aagiza msako wafugaji waliopiga watendaji Longido

Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kuwasaka na kuwakamata wafugaji wote wa Tarafa ya Engarenaibor waliohusika na tukio la kuwapiga watendaji wa serikali baada ya kukamata mifugo yao.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe.

Inaelezwa kuwa wafugaji hao wamefanya tukio hilo baada watendaji wa serikali baada ya kukamata mifugo pamoja na wahalifu waliokua wakitorosha mifugo hiyo kwa njia za panya  kuelekea Nchi Jirani ya Kenya kwa lengo la kukwepa kodi.

Mmoja wa watendaji hali yake mbaya na amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Longido kwa matibabu zaidi.

Taarifa zinasema mpaka sasa wanaoshikiliwa na jeshi la polisi ni Diwani wa Kata ya Matale, Mh Jamse Kokani na wananchi wanne ambao ni Paulo Orkeri,Yohana Olohngo,Kimani Laizer na Mathayo Salepi.

 

Habari Kubwa