DC Naano atoa onyo kwa wanaoharibu miundombinu ya maji

09Jul 2020
Dotto Lameck
Musoma
Nipashe
DC Naano atoa onyo kwa wanaoharibu miundombinu ya maji

MKUU wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano ametoa onyo kali kwa watu wanaoharibu na kuiba miundombinu ya maji huku akisisitiza kuwa Serikali haitamuonea huruma mtu yeyote atakayekamwatwa akihujumu miundombinu hiyo na watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

MKUU wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano.

Dk. Naano amesema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa maji Wilaya ya Musoma vijijini ambapo amesema miradi mingi ya maji vijijini inakufa kutokana na watu wasiowaaminifu kuiba na kuharibu miundombinu hiyo hali ambayo inakwamisha kufikia lengo la kumtua mama ndoo kichwani.

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa maji walioshiriki kikao hicho wameelezea hali ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo yao huku baadhi yao wakilalamikia maslahi kwa jumuia za maji vijijini kuwa ndiyo yanasababisha miradi hiyo ya maji kufa

Habari Kubwa