DC Sabaya awavaa wanaopandisha bei Barakoa na Sanitaizer

20Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
HAI
Nipashe
DC Sabaya awavaa wanaopandisha bei Barakoa na Sanitaizer

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameamuru maofisa biashara wilayani humo kuwakamata wafanyabiashara na kuyafunga maduka yote ambayo yatakayo bainika kupandisha bei ya Barakoa na Sanitaizer. 

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya.

Ameagiza kuanza mara moja kwa ukaguzi wa dharura katika maduka yanayouza vifaa vya kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19).

Ole Sabaya ameagiza kuanza kwa msako huo leo mchana, wakati akizungumza na viongozi wa dini kabla ya kuanza kwa ibada maalum ya kumuomba Mwenyenzi Mungu aliepushe taifa na janga la ugongwa huo ambalo sasa limesambaa na kuwa janga la dunia.

Soma zaidihttps://bit.ly/2wmL3Cg

                                                                      Sanitaizer.
                                                                                       Barakoa.

Habari Kubwa