DED Boniphace asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

20Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
DED Boniphace asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

WAZIRI wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Magesa Boniphace, kuanzia leo April 20, 2021 ili kupisha uchunguzi dhidi yake.

Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo kutoka kwa Wananchi na Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Hamisi Tabasamu.

Tuhuma hizo zimeelekezwa kwa Mkurugenzi na baadhi ya Wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo na zinaonesha kuwa Mkurugenzi kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara hizo wamekuwa wakifanya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za Umma zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Waziri Ummy amemuagiza pia Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuunda Timu ya Uchunguzi wa kuchunguza tuhuma hizo haraka.

Habari Kubwa