Deni la serikali lafikia bilioni 39

07Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Deni la serikali lafikia bilioni 39

Deni la serikali inalodaiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji limefikia Sh.bilioni 39.9 hadi mwezi Machi mwaka huu.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso

Kutokana na deni hilo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amezitaka taasisi za serikali zinazodaiwa kulipa madeni kwa mamlaka za maji nchini, ili ziweze kutoa huduma bora ya maji inayokidhi mahitaji ya wananchi.

Aweso ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA), alipotembelea mamlaka hiyo kwa dhumuni la kujionea utendaji wa mamlaka hiyo mkoani Kilimanjaro.

 

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mbele kulia) akiwa na Msimamizi wa Mradi, Mhandisi Richard Magwizi (kulia) wakipita kwenye moja sehemu ya mradi wa Same-Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

‘‘Mamlaka za Maji nchini zimeendelea kukabiliwa na changamoto ya malimbikizi makubwa ya madeni ya ankara za matumizi ya maji kwa taasisi za Serikali, ambazo zimekuwa zikipata huduma  ya maji na kushindwa kulipa kwa wakati, ambapo hadi kufikia Machi 2017 deni lilikuwa limefika Sh. bilioni 39.94’’, amesema Aweso.

 

Habari Kubwa