Dereva afariki ndani ya basi analoliendesha

20Mar 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Dereva afariki ndani ya basi analoliendesha

Dereva wa basi la Isamilo lenye namba za usajili T CQB 609, Sebastian Mathias (45), amefariki dunia akiwa ndani ya basi hilo, katika eneo la Tinde wilaya ya Shinyanga akitokea Mbeya kwenda Jijini Mwanza.

basi la Isamilo.

Tukio hilo limetokea leo Machi 20, 2020 majira ya saa 4 asubuhi wakati basi hilo likitokea Mbeya kwenda Jijini Mwanza ambapo walipofika eneo hilo la Tinde ndipo, wenzake wakamshusha na kumpeleka kwenye kituo cha afya Tinde na alipopimwa na daktari alikutwa ameshakufa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Deborah Magiligimba, amesema dereva huyo tangu anatoka Mwanza kwenda Mbeya inasemeka aisema ana jisikia vibaya, na wakati wa kurudi Mwanza kutoka Mbeya walipofika Singida ikabidi abadilishane na dereva mwezake.

“Dereva wa basi Kampuni ya Isamilo yenye namba T CQB 609 Sebastian Mathias mwenye umri wa miaka 45 amefariki dunia ndani ya basi, ambapo walipofika Tinde wenzake wakampeleka kwenye kituo cha afya Tinde, na alipopimwa na daktari akagundulika alikuwa ameshafariki muda mrefu,”amesema Magiligimba.

“Dereva huyo tangu anatoka Mwanza kwenda Mbeya alikuwa akidai kujisikia vibaya na wakati wa kurudi kutoka Mbeya kwenda Mwanza walipofika  Singida ikabidi abadilishane na dereva wa pili na walipofika Tinde ikabidi wenzake wamshushe kwenye kituo cha afya Tinde na alipopimwa alikuwa tayari ameshafariki dunia,” amesema 

Aidha amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika kituo hicho cha afya Tinde, ambapo abiria waliokuwa kwenye basi hilo wameendelea na safari yao kwenda Jijini Mwanza.

Habari Kubwa