Dereva taxi afariki kwa kusombwa maji

18Jan 2021
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe
Dereva taxi afariki kwa kusombwa maji

DEREVA taxi katika Jiji la Dodoma, Maxmilian Richard, amefariki dunia akiwa ndani ya gari lake, baada ya kusombwa na maji wakati akivuka korongo.

Dereva huyo aliyekuwa mkazi wa eneo la Nzuguni alisombwa na maji yaliyotokana na mvua inayoendelea kunyesha alipokuwa akivuka korongo linalounganisha eneo la Nzuguni A na B, jijini hapa.

Akizungumza na Nipashe, Diwani wa Kata ya Nzuguni, Aloyce Luhega, alisema alipigiwa simu majira ya saa 9:30 usiku na mmoja wa wananchi iliyoeleza kwamba kuna gari limesombwa na maji likiwa na mtu ndani.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa