Devotha Minja kutumia fedha za mfuko wa jimbo kufungua duka la dawa

21Sep 2020
Christina Haule
Morogoro
Nipashe
Devotha Minja kutumia fedha za mfuko wa jimbo kufungua duka la dawa

MGOMBEA Ubunge wa Morogoro Mjini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Devotha Minja, amesema akipata ridhaa ya kushika jimbo hilo atatumia fedha za miaka miwili za Mfuko wa jimbo Sh Mil 57 kwa mwaka kufungua duka la dawa kwenye geti la hospitali ya Rufaa mkoani hapa ili....

wananchi wapate dawa kwa wepesi na kwa bei rahisi.

Minja alisema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho zilizofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi k,ndege Manispaa ya Morogoro.

Alisema licha ya kuwa na hospitali, lakini upatikanaji wa dawa bado umekuwa mgumu na kwamba kwa kuweka duka la dawa la Serikali kutasaidia wananchi kupata dawa zote wanazoandikiwa hospitali.

Hata hivyo alisema, atahakikisha akiingia madarakani anajenga hospitali ya wilaya kwasababu haipo na kama ipo haina uwezo wa kutoa huduma ikiwemo upasuaji licha ya kuwa kwenye eneo ni mbali na makazi ya watu.

Naye Mgombea ubunge Wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, aliwataka wana Morogoro kumchagua Minja kuwa mbunge wao ili waone mabadiliko katika jimbo hilo.

Alisema akiwa mbunge mkoani Iringa ameweza kusimamia mengi na wana Iringa hawataki kumuacha aende na kwamba mazuri anayotenda yeye yatatendwa na Minja kwenye Manispaa.

Habari Kubwa