DiCoCo yatoa elimu ya kisukari, vipimo kwa wazee Bagamoyo

09Dec 2019
Na Mwandishi Wetu
Bagamoyo
Nipashe
DiCoCo yatoa elimu ya kisukari, vipimo kwa wazee Bagamoyo

Taasisi inayotoa elimu ya ugonjwa wa Kisukari kwa Jamii, DiCoCo imeendesha tamasha la kupima afya na kutoa elimu juu ya lishe bora kwa wazee Bagamoyo mkoani Pwani lililopewa jina la "Mtoko na Mzee".

Katika tamasha hilo DiCoCo ilishirikiana na Hospitali ya Kisukari na Moyo St. Laurent, Kampuni ya Bliss Pals Tanzania pamoja na Kampuni ya Communication for Impact.

Mkurugenzi wa DiCoCo, Lucy Johnbosco amesema lengo la tamasha hilo ni kuwakutanisha wazee na jamii zinazowazunguka ili kuongelea changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa za afya.

Mkurugenzi wa Bliss Pals Tanzania, Janeth Mghamba, amesema kuwa wazee wamekuwa wakisahulika mara kwa mara kwani wazee nao wana haki ya kutoka na kujumuhika pamoja na watu wengine, tifauti na ilivyozoeleka kwa baadhi ya familia zinazoishi na wazee kuwaacha nyumbani, jambo ambalo limeungwa mkono na Mkurugenzi wa Communication for Impact, Eliminatha Paschal.

Katika tamasha hilo wazee waliohudhulia walipata nafasi ya kupima kupima maradhi ya Kisukari na Shinikizo la damu na pamoja na kupata elimu ya lishe na ugonjwa wa kisukari zoezi ambalo lilisimamiwa na DiCoCo.

"Dhumuni la kuwa hapa na kushirikiana na wenzetu hawa ni kuwaonesha wazee wetu kuwa bado wana umuhimu kwetu lakini pia umri ni moja kati ya sababu ya Kisukari kwahiyo tukaona ni jambo jema wazee wetu wajue hali zao na kupata elimu ya maradhi ya Kisukari na Lishe bora" amesema Lucy Johnbosco, Mkurugenzi wa DiCoCo.

Habari Kubwa