Dk. Chaula akabidhiwa ofisi

21Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Dk. Chaula akabidhiwa ofisi

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Zainabu Chaula amekabidhiwa rasmi Ofisi ya Wizara na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii ambaye kwasasa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk.John Jingu.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma baada ya Rais Samia Suluhu Hassan,  kuiunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara Dk. Chaula, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kujituma katika kutekeleza majukumu yao. 

"Kila mmoja hapa ana karama yake, sasa tuunganishe hayo maarifa ya mtu mmoja mmoja tutembee pamoja" Dk. Chaula

Ameongeza kuwa, kiongozi ni wasifu katika eneo analofanya kazi na kuleta matokeo chanya kwenye eneno la utekelezaji wa majukumu yao hivyo, ni vyema kuhakikisha wanatumia vipawa vyao kusadia kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Habari Kubwa