Dk. Gwajima azindua mfumo wa ‘AfyaSS’

15Sep 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Dk. Gwajima azindua mfumo wa ‘AfyaSS’

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima, amezindua mfumo wa kidigitali wa usimamizi shirikishi kwenye huduma za afya (AfyaSS) na kugawa Vishikwambi 900 ili kutatua kero mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya afya.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima.

Mfumo huo uliozinduliwa leo umetengenezwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Shirika lisilo la Kiserikali la PATH kupitia mradi wa ‘Data use partnership’.

Akitoa maelezo ya mfumo huo, Mkuu wa Kitengo kidogo cha usimamizi shirikishi wa wizara hiyo, Dk.Chrisogone German, amesema kupitia mfumo huo utarahisisha uratibu na usimamizi wa shughuli za sekta ya afya, matumizi ya takwimu na ufuatiliaji wa mipango inayotekelezwa.

“Tumenunua Vishikwambi 900 ambavyo tutavigawa kwa halmashauri na mikoa ambapo kwa kila mkoa vishikwambi vitatu na kila halmashauri vishikwambi vitatu, tumetoa mafunzo kwa watumishi ngazi mbalimbali, ”amesema.