Dodoma kufanya kongamano kujadili kushuka kiwango cha elimu

06Mar 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Dodoma kufanya kongamano kujadili kushuka kiwango cha elimu

KUTOKANA na kushuka kwa kiwango cha ufaulu Mkoa wa Dodoma, unatarajia kufanya kongamano la siku mbili kwa wadau wa elimu ili kuangalia kero zinazosababisha hali hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge amesema kongamano hilo litafanyika Machi 21 hadi 22, mwaka huu na litafunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Amesema hali ya maendeleo ya elimu kwa Mkoa huo si nzuri huku akidai kuwa vipo baadhi ya viashiria vinavyosababisha kushuka kwa kiwango hicho ikiwemo wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Soma zaidi: https://bit.ly/2VXqRkK

Habari Kubwa