Dola mil. 425 kuboresha elimu ya juu

14Jan 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Dola mil. 425 kuboresha elimu ya juu

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB), inatarajia kutumia zaidi ya Dola za Marekani 425 kutekeleza mradi wa kuboresha elimu ya juu ya mabadiliko ya kiuchumi (HEET).

Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu ya mabadiliko ya kiuchumi (HEET) kwa wanufaika wa moja kwa moja wa taasisi za serikali, Katibu Mkuu, Dk. Leonard Akwilapo, alisema mradi huo ni muhimu kwa kuwa utaleta mabadiliko makubwa ya kitaaluma nchini.

Alisema kikao kingine cha wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali kitafanyika leo lengo ni kupata maoni ya wadau katika maboresha na utekelezaji wa miradi huo na wanataaluma, na kesho kutakuwa na kikao cha wadau wengine.

Kwa mujibu wa Dk. Akwilapo, mradi huo unakuja kujibu changamoto za elimu zilizopo nchini na kuishukuru WB kwa kufadhili mradi unaotambua mahitaji ya nchi katika sekta ya elimu.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa