EAC yajipanga kudhibiti magojwa ya mlipuko mpakani

22May 2019
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
EAC yajipanga kudhibiti magojwa ya mlipuko mpakani

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) inatarajia kufanya zoezi la majaribio ya kudhibiti magonjwa ya mlipuko eneo la mpaka wa Namanga upande wa Longido Nchini Tanzania na Kajado nchini Kenya ifikapo Juni 11-14 mwaka huu.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashari, Dk. Michael Katende.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwakilishi wa Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashari, Dk. Michael Katende ambaye ni Mkuu wa Idara ya Afya Jumuiya hiyo hapo jana katika ukumbi Wa kituo kimoja cha Forodha (OSBP) upande Wa Kenya.

"Zoezi hili la kudhibiti magonjwa yalipuko maeneo ya mpakani ni makubaliano ya mawaziri wa afya wa jumuiya ya afrika mashariki mwaka 2015" alidai

Hata hivyo alieleza kuwa zoezi hili linawezeshwa na shirika la maendeleo ya jamii nchini ujerumani GIZ pamoja na shirika la afya duniani WHO lenye mamlaka ya kutekeleza kanuni za afya kote kimataifa duniani ,Kwa kushirikiana na Jumuiya ya afrika mashariki (EAC).

Alisema kuwa kumekuwa na magonjwa ya mlipuko maeneo ya mipakani kutokana na mwingiliano Wa watu ,na wakati mwingine magonjwa hayo husambazwa na wanyama na binadamu ,na uleta athari katika sekta ya utali,Biashara na kilimo.

Hivyo kwa sasa wanaangalia utayari Wa Nchi hizo mbili katika kukabiliana na magonjwa hayo na kuweka njia m'badala ya kudhibiti pindi yanapotokea,kwani magonjwa hayo husababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi na hata maendeleo ya wananchi.

Magonjwa hayo yanayoonekana kuwa tishio na kupoteza maisha ya watu wengi kwa haraka katika kanda ya afrika mashariki ni Ebola,Homa ya bonde la ufa,kipindupindu,kupooza ,ugonjwa wa Tauni pamoja na kichaa cha Mbwa.

Alisema kuwa,wanatarajia kukutana na watu zaidi ya 250 kutoka upande zote mbili za nchi hizo kwa ajili ya zoezi hilo la June ,lakini pia kutakuwepo na wengine kutoka ndani ya Umoja wa afrika mashariki ,hata hivyo kila nchi inatarajia kuwa na watu maalumu watakao shughulikia magonjwa hayo yalipuko maeneo ya mipakani.

Aliwataka wananchi na wasafiri mbalimbali wanaopita kupitia mpaka huo kuondoa hofu ifikapo June 11 kwani zoezi hilo litakua likifanyika katika maeneo mbalimbali iliwemo katika kituo hicho cha Forodha upande wa Tanzania na Kenya(OSBP),vituo vya afya,vichinjio na mashamba,majeshi na polisi,vyombo vya habari pamoja na wananchi kutoka pande zote mbili za nchi hizo.

Mratibu wa sekta ya afya ya jumuiya ya afrika mashariki katika Wizara ya mambo ya nje na ushitikiano wa afrika mashariki Edward Komba ambaye ni mwakilishi wa Upande wa Tanzania katika zoezi hilo, Alisema kuwa tukio hili linalotarajiwa kufanyika June ni makubaliano ya baraza la 11 la mawaziri wa afrika mashariki

Alieleza kuwa jumuiya inakua kwa kasi ,na ongezeko la watu ni kuwa,hivyo magonjwa hayo husambaa kwa mwingiliano baina ya watu ,na kwa upande wa Tanzania wameshajipanga namna ya kudhibiti magonjwa hayo

Alidai kuwa zoezi hili limeshirikisha Wizara ya afya,kilimo ,Mifugo, utali pamoja na wizara ya mambo ya ndani ya nchi na wadau mbali mbali ,na lengo hasa ni kila nchi mwanachama wa jumuiya ya afrika mashariki kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko yanapotokea.

Habari Kubwa