ECOWAS kujadili mzozo wa Mali

30May 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
ECOWAS kujadili mzozo wa Mali

VIONGOZI wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), wanatarajia kukutana leo Jumapili nchini Ghana kwa ajili ya kujadili mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Mali.

Viongozi hao wataamua kuhusu hatua ya kuchukua kufuatia mapinduzi ya pili katika kipindi cha miezi 9. Kiongozi wa kijeshi wa Mali Kanali Assimi Goita amealikwa kuhudhuria kikao cha mashauriano hapo jana kabla ya kuanza kwa mkutano wa leo wa kilele.

Goita amehudumu kama Makamu wa Rais tangu alipoongoza mapinduzi mwezi Agosti mwaka uliopita yakumuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Ibrahim Boubacar Keita.

Hata hivyo, ECOWAS inahofia mabadiliko hayo yanaweza kuyumbisha utulivu na kudhoofisha mapigano ya Kikanda dhidi ya vikundi vinavyohusiana na Al-Qaeda na ISIS.

Nafasi ya Rais na Waziri Mkuu zimekuwa zikishikiliwa na viongozi wa kiraia, Bah Ndaw na Moctar Ouane kufuatia shinikizo kutoka kwa jumuiya ya ECOWAS ambayo imekuwa mpatanishi.

Habari Kubwa