Edward Lowassa arejea CCM

01Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Edward Lowassa arejea CCM

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi leo Machi mosi 2019 na kupokelewa na mwenyekiti wa chama hicho Rais Magufuli.

Mwenyekiti wa CCM , John Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, ambaye amekitosa leo chama cha CHADEMA na kuamua kurejea CCM.

Akizungumza wakati wa kumpokea Lowasa, Rais Magufuli amesema kuwa kiongozi huyo alikwenda CHADEMA kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

"Ndugu yetu amerudi na ametueleza sababu zilizomuondoa kuwa zilikuwa nje ya uwezo wake", amesema Rais Magufuli.

Aidha amesema kuwa baada ya kutafakari kwakina ameamua kurejea nyumbani, hivyo wameamua kumpokea.

Lowassa alitimkia CHADEMA mwaka 2015 baada ya kukatwa jina lake na Kamati Kuu ya CCM katika kinyang'anyiro cha kugombea Urais.

Soma zaidi: https://bit.ly/2GSHyaw

Habari Kubwa