Ekari nne na nusu za bangi zateketezwa Arumeru

22May 2022
Na Mwandishi Wetu
Arumeru
Nipashe Jumapili
Ekari nne na nusu za bangi zateketezwa Arumeru

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limeteketeza Ekari nne na nusu za bangi katika eneo la Kisimiri juu, katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru mkoani humo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Gaudianus Kamugisha, amesema May 21, 2022 wameteketeza bangi yote iliyokuwa shambani na nyumbani ambayo ni kiasi cha gunia 10 pamoja na debe moja la mbegu ya bangi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya vijiji.

Amesema operesheni hiyo ni mwendelezo wa operesheni zinazofanyika mara kwa mara katika Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kupambana na kilimo cha bangi pamoja na watumaji wa bangi.

Kamugisha amesema watuhumiwa wanaoishi katika nyumba hizo (maboma) yalikopatikana magunia ya bangi hizo walikuwa tayari wameshakimbia katika nyumba zao, hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao.

Habari Kubwa