Elimu ya sheria yaongezeka kwa asilimia 66 Simiyu

07Aug 2020
Happy Severine
Simiyu.
Nipashe
Elimu ya sheria yaongezeka kwa asilimia 66 Simiyu

Uelewa wa wananchi juu ya masuala ya sheria  Mkoani Simiyu umeongezeka kwa asilimia 66 na asilimia 10 ya mwaka 2016 kabla ya kuanza kwa   mradi wa upatikanaji endelevu wa msaada wa kisheria Mkoani Simiyu.

wananchi waliojitokeza katika banda la Kasodefu kujipatia elimu ya sheria.

Hayo yamebainishwa jana na Afisa  ufuatiliaji na tahimini wa shirika lisilo la kiserikali la Kasodefu, John Titus wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari  katika maonesho ya nane nane  yanayoendelea kufanyika viwanja vya nane nane Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Titus amesema mwitikio  wa  wananchi juu ya masuala ya sheria umeongezeka kwa kiwango kikubwa kutokana na elimu inayoendelea  kutolewa na  shirika hilo.

Titus amesema kuwa ongezeko hilo la uelewa limesaidia kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili kwenye vyombo husika.

Ameongeza kuwa kwa kipindi cha siku nane za maonesho ya nane nane wamefanukiwa kutoa elimu ya sheria kwa wananchi wapatao 1900 na kati ya hao 56 wanahitaji kusaidiwa huduma za kisheria.

Habari Kubwa