Ewura yataja sababu uhaba wa mafuta

04Aug 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Ewura yataja sababu uhaba wa mafuta

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imesema tatizo la upatikanaji wa mafuta ya Petroli limetokana na kuchelewa kwa Meli moja iliyotakiwa kufika nchini kati ya Julai 22 na 24, mwaka huu.

Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo.

Hata hivyo, Meli hiyo imewasili Julai 29, mwaka huu na inaendelea kupakua mzigo huku zingine tatu zikitegemewa kuwasili kati ya Agosti 17 na 31, mwaka huu zenye lita Milioni 100.075 zitakazotosheleza mahitaji ya nchi kwa siku 22.

Akizungumza Leo na Waandishi wa Habari, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo, amesema kuchelewa kwa meli hiyo kumetokana na upepo wa Monsoon baharini hali iliyofanya meli kusafiri kwa kasi ndogo.

"Kutokana na kuchelewa kwa meli hiyo kwa takriban siku saba kuna uhaba kidogo uliojitokeza katika maeneo machache, hata hivyo Ewura ilifanya mawasiliano na Kampuni za Mafuta kuhakikisha mafuta yanapatikana maeneo yote,"amesema.

 

Habari Kubwa