Gari la maiti lakamatwa na dawa kulevya katika jeneza

14Jan 2021
Boniface Gideon
Tanga
Nipashe
Gari la maiti lakamatwa na dawa kulevya katika jeneza

KIKOSI Maalum cha Jeshi la Polisi mkoani Tanga, kimenasa dawa za kulevya zenye uzito wa kilogramu 133 (mabunda 1,685) zikisafirishwa huku zikiwa zimefichwa ndani ya mifuko sita ya sandarusi iliyowekwa kwenye gari la kusafirishia maiti.

Limesema mifuko hiyo ya sandarusi yenye dawa hizo imekutwa ndani ya jokofu ambalo huwekwa jeneza lenye mwili wa marehemu.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Blasius Chatanda, alisema jana kuwa dawa hizo zilikamatwa Januari 12 mwaka huu majira ya saa mbili usiku katika Kijiji cha Manga, Kata ya Mkata, Wilaya ya Handeni.

Alisema gari lililohusika kuzisafirisha dawa hizo ni aina ya Volvo lenye namba za usajili T 569 DSZ, mali ya Kampuni ya Nuru Funeral Service ya Dar es Salaam.

"Tuliyemkamata ni dereva wa gari hilo la kubeba maiti, Simon Tarimo (37), mkazi wa Kimara, Dar es Salaam. Huyu alikuwa akisafirisha mirungi akiwa ameweka kwenye jokofu linalotumika kuhifadhia jeneza lenye maiti wakati wa kusafirisha.

“Hizo dawa za kulevya, zilikuwa zimehifadhiwa kwenye mifuko sita ya sandarusi," kamanda huyo alisimulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Chatanda, dawa hizo zilikuwa zikisafirishwa kutoka Usangi, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwenda jijini Dar es Salaam...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa