GDSS waiomba serikali kuelimisha wachimba madini

26Sep 2021
Yasmine Protace
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
GDSS waiomba serikali kuelimisha wachimba madini

​​​​​​​WASHIRIKI wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), wameiomba serikali iendelee kutoa elimu kwa wachimba madini ili waweze kunufaika na madini hayo.

Hayo yamesemwa na mmoja wa washiriki wa semina hizo za GDSS Hawa Juma, wakati alipokuwa akichangia mada iliyokuwa ikisema taarifa za mapato katika sekta ya madini.

Amesema madini yapo ya aina mbalimbali na yanaliletea taifa mapato, lakini kinachotakiwa kuwepo na utaratibu ambao unatakiwa kufanyika wa kutoa taarifa za mapato yanayopatikana ikiwamo na uuzwaji wake.

"Elimu bora inapotolewa kwa wachimbaji itasaidia hata soko kuwa kubwa, ambapo mchimbaji ananufaika pia serikali nayo itanufaika kupitia mapato hayo” amesema Hawa.

Amesema yapo ya aina mbalimbali na yapo maeneo mbalimbali, hivyo serikali iwaandae mazingira mazuri ya uchimbaji kwa wanawake ili kuwaepusha na masuala ya ukatili wa kijinsia.

Ameongeza kuwa kuna machimbo yapo porini, hiyo inatakiwa miundombinu kwa wanawake iangaliwe upya.

Amesema elimu ikitolewa mara kwa mara itawasaidia wachimbaji kutorubuniwa na madalali wanaofika vijijini kununua madini hayo kwa bei ndogo.

Joyce Mkina kutoka TGNP Mtandao, amesema kuwa Tanzania inatekeleza sheria ya madini .

Amesema Kuna sheria ya mwaka 1867 na IPO ya mwaka 2007.

Amesema sera hiyo ya madini ya mwaka 2007 ikaanza kutekelezwa mwaka 2010.

Malengo ya deta yanalenga ongezeko la dhamani ya madini ikiwamo kukuza mapsto.

Ameongeza kuwa lengo lingine ni kukuza uchimbaji mdogomdogo ambapo sera hiyo ililenga kukuza uchumi kwa wawekezaji.

"Kutokana na sera hizo fursa zinatakiwa kupatikana katika madini ili kusaidia kuongezeka kwa mapato",amesema.

Habari Kubwa