Moshi wazuia wafanyabiashara kuendelea na biashara Kariakoo

11Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Moshi wazuia wafanyabiashara kuendelea na biashara Kariakoo

KUTOKANA na eneo kubwa kuungua katika soko kuu la Kariakoo mkoani Dar es Salaam kutaendelea kuwa na moshi usiyofaa ambayo haitawawezesha Wafanyabiashara kufanya shunguli zao hadi pale watakapopewa taarifa rasmi.

Hayo yamesemwa leo Julai 11, na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, wakati alipotembelea soko hilo kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kuangalia eneo lililoshika moto.

Masunga amesema hadi kufikia kesho haitawezekana wafanyabiashara kuendelea na shuguli zao kutokana na uwepo wa gesi ambayo haifai.

“Nimefika hapa kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kuangalia eneo lililoshika moto, kwa kweli nimeshuhudia moto ulikuwa ni mkubwa sana na kazi ya kuzima moto huo ilifanyika vizuri kwa kuwa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji lilikuwa limejiandaa vilivyo.

“Tulipata changamoto mbili wakati wa kuzima moto, kwanza hapa katika soko la Kariakoo sehemu za kuchukulia maji hazitoi maji, hivyo ilitubidi twende mbali kwa ajili ya huduma hiyo na tatizo la pili ni watu kuzingira eneo la tukio hali iliyosababisha magari yetu kushindwa kuingia na kutoka kwa urahisi,” amesema Masunga.

Aidha, Masunga amesema kazi ya kuzima moto imekamilika na kinachofuata hivi sasa ni uchunguzi wa chanzo cha moto huo.

Habari Kubwa