Guterres aapishwa muhula wa pili

19Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Guterres aapishwa muhula wa pili

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameapishwa jana kuhudumu muhula wa pili na wa mwisho kama Katibu Mkuu wa chombo hicho cha kimataifa, akiahidi kujifunza kutokana na janga la Covid-19.

Katibu mkuu huyo amesema wataendeleza mpango endelevu wa ufufuaji uchumi wa haki, usawa na unaojali mazingira na kuimarisha ushirikiano wa kimaitaifa katika kushughulikia maswala yanayoukabili ulimwengu.

Guterres ameahidi kutoegemea upande wowote wa nchi wanachama na mashirika wakati wa shughuli ya kuapishwa kwake iliyofanyika Mjini NewYork.

Rais wa zamani wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa alihudhuria sherehe hiyo akiwa kiongozi wa kwanza wa serikali kufika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa tangu kuzuka kwa janga la Covid-19 mwaka mmoja uliopita.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amempongeza Guterres na kusema nchi yake itaendeleza ushirikiano thabiti na katibu mkuu huyo.

Habari Kubwa