Dk. Dorothy Gwajima alitoa agizo hilo jana wakati wa kikao na viongozi hao kwenye Ukumbi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Alisema vyama, bodi na mabaraza ya kitaaluma ndiyo wasimamizi wakuu na wadhibiti wa maadili na weledi, akibainisha kuwa wananchi bado wanakutana na vikwazo vingi vya maadili na weledi wakati wakisaka huduma za afya.
"Kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ukurasa 137, imeandikwa kushirikiana na vyama vya kitaaluma vya kada ya afya katika kusimamia uzingatiaji wa maadili na weledi katika utendaji wa watumishi, hilo ndiyo tunalotekeleza," alisema...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com