"Hakuna kuvaa tai nyekundu bungeni leo jioni"

22Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
DODOMA
Nipashe
"Hakuna kuvaa tai nyekundu bungeni leo jioni"

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kuzingatia itifakia hususani katika uvaaji bungeni, ambapo amewashauri wabunge kutokuvaa tai nyekundu leo wakati Rais Samia Suluhu Hassan wakati akilihutubia bunge.

Kauli hiyo ameitoa leo bungeni, mara baada ya kuhitimisha kipindi cha maswali na majibu ambapo amesema anapokuja kiongozi hususani mkuu wa nchi haishauriwi mtu mwingine kuvaa tai nyekundu. "Ningependa kuwakumbusha ndugu wabunge siku anayokuja kiongozi mkuu wa nchi basi haishauriwi sana kwa wenzangu mimi kuvaa tai nyekundu, nadhani tumekubali ile red inabakia na mwenye mamalaka, ni vizuri kuyajua hayo mambo jioni tutakaporudi na tai nyekundu utarudia geti la nje," amesema Ndugai.

Leo alasiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kulihutubia bunge pamoja na kutoa mwongozo wa serikali yake ya  awamu ya sita, bungeni Dodoma.

Habari Kubwa