Halmashauri Manyoni hampo 'serious' katika mradi mashamba ya korosho

10Feb 2024
Nipashe
Halmashauri Manyoni hampo 'serious' katika mradi mashamba ya korosho

MBUNGE wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Tabora, Hawa Mwaifunga amesema Halmashuri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida haiko 'serious' katika Mradi wa Kupanga,Kupima na Kumilikisha Mashamba ya Korosho...

...ambao serikali kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliikopesha halmashauri hiyo zaidi ya Sh.bilioni 1.5.

 

"Mkurugenzi hizi fedha tunazihitaji kama tulivyokubaliana,fedha hizi ni za wananchi zinahitajika na sehemu nyingine msifikiri ni Manyoni tu ambao mnazihitaji,haiwezekani tangu 2021 ni karibu miaka minne sasa hamuonyeshi dalili kuzirejesha angalie tusije tukakosesha bajeti yenu,"amesema hayo leo (Februari 10,2024) baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge TAMISEMI ilipotembelea mradi huo.

 

Naye Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Justin Kamonga, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kuweka mkakati wa kurejesha hizo walizokopeshwa. 

 

Aidha, kamati hiyo imeiagiza halmashuri hiyo kutoa taarifa inayojitosheleza ambayo itaeleza kwa kina kuhusu mradi huo ili kujua changamoto na kama kuna matatizo ieleze ni nani alisababisha hilo na hatua gani zimechukuliwa.

 

"Kufiatia maelezo yaliyopi kwenye taarifa mliyotusomea kamati inashindwa kushauri kuhusu mradi huu kwa hiyo tunaitaka halmashauri iwasilishe taarifa nyingine kwa kamati kabla ya vikao vya bajeti havijaanza mwezi Machi 2024,pia fedha hizi ni mkopo tunahitaji mkakati wa halmashauri wa jinsi ya kuzirejesha" amesema.