Halmashauri ya Maswa yatatua changamoto soko la viazi lishe

29May 2020
Happy Severine
Massa
Nipashe
Halmashauri ya Maswa yatatua changamoto soko la viazi lishe

Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha viazi lishe ambacho kitatua changamoto ya soko la wakulima wa zao la viazi lishe hapa nchini.

baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha viazi lishe Wilayani Maswa wakiwa katika eneo la maandalizi ya kukausha viazi.

Mbali na kutatua changamoto hiyo ya wakulima pia kitapunguza utegemezi wa mapato kutoka serikalini na kutoa fursa za ajira  kwa vijana na wananchi.

Akisoma taarifa fupi leo ya ujenzi wa kiwanda hicho wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dk. Fredrick Sagamiko, amesema Kiwanda hicho  chenye chenye thamani ya shilingi Mil. 461 kina uwezo wa kukausha viazi tani moja na nusu kwa siku.

Aidha Dk. Sagamiko amesema  mbali na ukamilishaji wa kiwanda hicho, bado wanakabiliwa na vikaushio ( Solar dryier) pamoja na uhaba wa fedha za mtaji wa uendeshaji wa kiwanda .

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, ameridhishwa na uwekezaji huo na kuwaelekeza shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda Tanzania Tirido kuleta mara moja nishati mbadala kwa kiwanda hicho ili kuongeza uzalishaji.

Kiwanda cha viazi lishe kwa sasa soko lake lipo katika Mikoa ya Singida, Iringa, Dodoma, Shinyanga na Mara.

Habari Kubwa