Kichere ameyasema hayo leo Jumapili, Machi 28, 2021 mbele ya Rais Samia wakati akikabidhi ripoti aliyoifanya kwa taasisi za Serikali Kuu, mamlaka ya serikali za mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na vyama vya siasa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ulioishia Juni 30, 2020.
“Tumeongeza mashirika 10 ambayo tunayakagua na nimeshirikiana na makampuni mengine binafsi kuhakikisha tunakagua ipasavyo pia tumefanya kaguzi za kitaalamu SGR, miundombinu mabasi yaendayo haraka, barabara kuu Morogoro, Kibaha, miradi ya maji Wilaya ya Same na Korogwe,” amesema CAG Kichere.
“Hati 243 za serikali kuu 235 zinaridhisha na nyingine sita zina mashaka, mamlaka ya Serikali za mitaa ni 185 na kati ya hizo 124 zinaridhisha na zenye mashaka 53 na 8 zimekutwa ni mbaya.