Hatma rufaa ya Mbowe, Matiko kesho

28Feb 2019
Hellen Mwango
Dar es Salaam
Nipashe
Hatma rufaa ya Mbowe, Matiko kesho

Hatma ya kusikilizwa rufani ya kupinga kutenguliwa dhamana ya Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chedema) freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko kujulikana kesho.

Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watatu Februari 18, mwaka huu ilisikiliza rufani ya Jamhuri ya kupinga Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza maombi ya vigogo hao wa Chadema.

Kesho Mahakama ya Rufaa itatoa hukumu yake kama washtakiwa wasikilizwe au la.

Wakati huohuo kesi ya jinai inayowakabili Mbowe na wenzake wanane imepigwa kalenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Machi 13, mwaka huu itakapotajwa.

Habari Kubwa